Katibu mkuu
wa Wizara ya Habari,Vijana Utamaduni na Michezo Bw. Sethi Kamuhanda
(katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
jana jijini Dar es salaam kuhusu matumizi ya nembo ya miaka 50 ya Uhuru
wa Tanzania Bara na maonesho makubwa ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania
Bara yatakayofanywa na Wizara hiyo eneo la Butiama, Musoma kuanzia
tarehe 7-14 Oktoba na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki
maonesho hayo na kuitumia nembo hiyo kwenye shughuli mbalimbali
zikiwemo za biashara .Kushoto ni Bw. Mulwa Msongo Mkurugenzi wa
Utawala na Rasilimali watu na Bw. Raphael Hokororo (kulia) Mkurugenzi
msaidizi wa Idara ya Habari.
Msanii na
kiongozi wa B. Band Banana Zolo (kushoto) akiongea na waandishi wa
habari (hawapo) pichani kuweka msisitizo wa ushiriki wa wasanii wa
kizazi kipya na wale wakongwe katika Tamasha la pamoja la maadhimisho
ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara jana jijini Dar es salaam.
Wengine ni Said Fella mwakilishi wa kundi la TMK Family (wa pili kutoka
kushoto),Mzee King Kii (katikati) na Bw. Waziri Ally.Picha na Aron
Msigwa – MAELEZO.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)