Wajumbe
wa Kamati Teule iliyoundwa na Bunge kuchunguza sakata la aliyekuwa
katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Ndg. David Jairo ikiwa kwenye
kikao chake leo jijini Dar es Salaam.Picha na Owen Mwandumbya-Bunge
---
Wajumbe wa Kamati Teule iliyoundwa na Bunge
kuchunguza sakata la aliyekuwa katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini Ndg. David Jairo kuchangisha pesa kwa ajili ya kupitisha Bajeti
ya Wizara pamoja na hatua ya katibu Mkuu kiongozi kuitolea taarifa ya
uchunguzi mbele ya waandishi wa Habari kabla ya kuwasilishwa Bungeni
imeanza kukutana leo katika Ofisi ndogo ya Bunge chini ya uenyekiti wa
Mhe. Injinia Ramo Makani (CCM), mbunge wa Tunduru Kaskazini,
.
kamati hiyo
inayoundwa na mhe. Goesbert Blandes (CCM), Mbunge wa Karagwe, mhe.
Mchungaji Israel Natse (Karatu-Chadema), mhe. Khalifa Suleiman Khalifa
(Gando-CUF) na mhe. Martha Jachi Umbulla (CCM). Mbunge wa Viti
Maalum, inafanya kazi kwa kuongozwa na hadidu tano za rejea ambazo ni:
kuchunguza
utaratibu uliobainika wa kukusanya fedha kwa ajili ya kukamilishwa kwa
uwasilishaji wa Hotuba za bajeti za wizara bungeni na kwamba, hadidu
hiyo ya kwanza itakuwa na vipengele vitatu. Vipengele hivyo ni pamoja
na:
·kuchunguza
uhalali wa utaratibu huo kisheria na kwa mujibu wa kanuni, iwapo fedha
hizo huwa zinakasimiwa katika bajeti husika pamoja na matumizi halisi
ya fedha zilizokusanywa.
Hadidu rejea ya pili ni kupitia taarifa ya
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu uchunguzi
alioufanya kuhusiana na agizo la Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini kuchangisha fedha taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kwa ajili
ya kufanikisha uwasilishaji wa Bajeti ya Wizara hiyo Bungeni,
Hadidu rejea ya tatu ni kuchunguza mfumo wa
Serikali kujibu hoja zinazotolewa bungeni na taratibu za kuarifu Bunge
matokeo ya utekelezaji wa hoja hizo". Hadidu rejea hiyo ya nne ina vipengele
viwili ambavyo ni kuchunguzwa kwa usahihi wa utaratibu uliotumiwa na
Katibu Mkuu Kiongozi kwa suala la Jairo na kubaini iwapo utaratibu huo
umeathiri dhana ya haki na madaraka ya Bunge.
Hadidu ya rejea ya tano ni kuangalia nafasi
ya Mamlaka ya Uteuzi kwa ngazi za Makatibu Wakuu katika kushughulikia
masuala ya nidhamu ya anaowateua na ya mwisho inawaelekeza wajumbe wa
Kamati hiyo kuangalia mambo mengine yoyote yenye uhusiano na uchunguzi
huo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)