Hili ndilo Lori lililochinja wafanyabiashara 14 Mbeya
Hivi Ndivyo ilivyotokea Mbeya jana
JINAMIZI la ajali za barabarani zimeendelea kumaliza watu Mkoani Mbeya,baada ya watu 14 wafariki dunia na wengine 41 kujeruhiwa vibaya baada ya gari aina ya Mitsubish Fuso waliyokuwa wakisafiria kutoka mnadani wilayani Chunya mkoani hapa kupinduka.
Waandishi wa mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kutoka Mbeya Moses Ng'wat na Esther Macha wanaripoti kuwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Anacret Malindisa, alisema tukio hilo la ajali lilitokea Septemba 24 mwaka huu majira ya 9;30 alasiri katika eneo la kijiji cha Msangamwelu wilaya ya Mbeya vijijini barabara ya Chunya-Mbeya.

Alisema
watu 11 walifariki dunia papo hapo,ambapo maiti zao zilipelekwa katika
Hospitali za Rufaa Mbeya na ile Teule ya Mbeya Vijijini ya Ifisi
Aliwataja waliokufa papo hapo ambao miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya ambao wametambuliwa kwa jina moja moja kuwa ni Exzavery, Kaloli, Lembo, Masai, Kashinje, Noa,mama Anna Ugalahenga, Mwakalasya, Meshack na Mwakilasa ambao miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.

Malindisa alisema
majeruhi 37 wamelazwa katika Hospitali ya Teule ya Ifisi wakati majeruhi
wengine wanne wamehifadhiwa katika hospitali ya Mwambani iliyopo mji wa
Mkwajuni wilayani Chunya. Kwaupande wa waliofia hospitali teule ya
Ifisi, Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo, Rhoda Kasongwa, aliwataja
waliokufa kuwa ni Emilia Mwangove (40), mkazi wa Mbalizi, Grasiano
Kalinga (37) na Msafiri Tinda (35) wote wakazi wa Mwanjelwa mjini Mbeya.
Kaongwa pia aliwataka majeruhi waliolazwa katika hospitali hiyo kuwa ni Mussa Mwangowe (27),Juma Mwambene (24),Msafiri Msangawale (20),Nelson Mwanyakule (45), Enock Saimon (28),Daudi Sanga (32),Aliko Mwakanjwanga (36), Daudi Joramu (3) Juma Mwakatobe (25), Satieli Kiwasi (45), Stany Elias (230 ,Charles Sanga (33), Mussa Ezekiel (27), Stwen Mwaibeju (25), Maiko Siwale (30), Estron Chaula (21),Amina Mwanyakule (42),Mbonis Kapoka (27) na Atu Mnkwama (63) wote wakazi wa Mbalizi.
Wengine ni Amani Emanuel (23) mkazi wa Songwe, Aneth Asangalwisye (43) mkazi wa Ilemi, Kachele Kasekenya (36) mkazi wa Mwanjelwa, David Mwakalasya (52) mkazi wa Air port, Nico Kessy (22) mkazi wa Utambalila,Leonard Paul (41) mkazi wa Ilemi, Daudi Sanga (29) mkazi wa Air port, Likugulan Lolamatu (35) mkazi wa Uhindini,Robart Mwalyambi (25) mkazi wa Makunguru, Adreano William (33) mkazi wa Mwanjelwa na Jenipher Mafupa mkazi wa Mwanjelwa.
Majeruhi wengine waliolazwa hospitali teule ya Ifisi ni Aneth Kajenga (43) mkazi wa Ilemi, Fausta Ndelwa (26) mkazi wa Iyunga,Hadija Hussein ( 42) mkazi wa Chunya, Ikupa Nobwa (39) mkazi wa Chunya,Victor Sondanki (42) mkazi wa Mbeya,Hilda Juma (40) mkazi wa Mbeya na Lukia Andrea (23) mkazi wa Air port.
Muuguzi Mkuu wa Hospitali Teule ya Ifisi, aliwataja majeruhi watatu ambao hali zao ni mbaya na wamehamishiwa katika hospitali ya Rufaa Mbeya kuwa ni Amina Mwanyakule, Aneth Kajenga na Eliud Kalekenya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya alisema gari hiyo yenye namba za usajiri T 532 AJF iliyokuwa ikiendeshwa na Kasenti Kapusi ilipinduka na kuacha njia baada ya dereva wake ambaye ndiye mmiliki wa gari hilo mkazi wa Iwambi jijini Mbeya kumshinda kukata kona na hivyo kupinduka
Alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi ambapo dereva huyo kutokana na gari hilo kubeba mizigo na abiria kupita kiasi ilimshinda wakati akijaribu kukata kona.
Malindisa
alisema Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limekuwa likijitahidi sana siku
za minada kuimalisha ulinzi kwa kuhakikisha magari yanayokwenda huko
yasibebe abiria na mizigo lakini madereva wamekuwa wakitumia mbinu
mbalimbali kuwakwepa askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani kwa kupita
njia vijijini ambazo siyo rasmi.Picha/Habari Kwa Hisani Ya Francis Godwin
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)