Askari Polisi wakimdhibiti kijana ambaye alifanya fujo kwa
kupiga mawe vioo vya benki ya CRDB tawi la Azikiwe, Posta Mpya, Dar es
Salaam jana na kusababisha wateja na wananchi kukimbia ovyo. (PICHA
ZOTE NA KASSIM MBAROUK)
wewe unajifanya fara sio, basi mimi ni fara zaidi...
Kaa chini...arrraaaaah!
Na Kamanda Mwaikenda
TAFRANI kubwa ilitokea jana katika Benki ya CRDB, tawi la
Azikiwe, baada ya kijana mmoja aliyehisiwa kuwa jambazi kurusha mawe
kwenye vioo vya benki hiyo na kusababisha wateja kukimbia ovyo
wakidhani wamevamiwa.
Tukio
hilo lilitokea jana mchana, ambapo kijana huyo anayedhaniwa kuwa akili
yake imeathirika kwa kubuia dawa la kulevya 'Teja' kurusha mawe
kuelekeza kwenye jengo hilo na kuvunja vioo.
Baadhi
ya wateja walianza kutimua mbio kutoka nje huku wengine wakilala chini
kuhofia maisha yao.Baada ya kuona hivyo, Polisi waliokuwa kwenye lindo
la benki hiyo, walifyatua risasi juu wakidhani majambazi wamevamia
benki hiyo. Lakini baada ya muda walimuona kijana huyo aliyekuwa
katikati a Barabara ya Azikiwe karibu na kituo cha Daladala cha Posta
Mpya, akiendelea kurusha mawe.
Polisi walimuendea
na kufanikiwa kumdhibiti na kuanza kumpatia mkong'oto wa nguvu, huku
wanachi wenye hasira wakitaka nao waruhusiwe kumwadhibu.
Ndani
ya benki hiyo hali ilikuwa shaghalabaghala, kwani mitungi ya maua na
baadhi ya nyaraka zilitawanyika ovyo, huku wakioneakana baadhi ya
wateja wakiwa wamezirai na wengine wakilia baada ya kupotelewa na
nyaraka muhimu za benki vikiwemo kadi na fedha taslimu.
Wakati
tukio hilo ilitokea, pia hali haikuwa nzuri kwa wafanyakazi wa benki
hiyo, kwani baadhi walisikika kuwa walipatwa na hofu kubwa kiasi cha
baadhi yao kukimbilia kujificha vyooni na kuacha kaunta zao.
Habari Kwa Hisani Ya Issa Michuzi - Michuzi Blogu





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)