Viongozi wa
waasi wa Libya wamewapa majeshi yanayomwuunga mkono Kanali Gaddafi mpaka
Jumamosi kusalimu amri au kukabiliana na majeshi. Mustafa Abdul Jalil,
anayeongoza Baraza la Mpito la Taifa (NTC), alisema onyo hilo
limeelekezwa kwa wanaomtii Kanali Muammar Gaddafi waliopo mji
alipozaliwa wa Sirte na katika miji mengine. Tangazo hilo limetolewa
baada ya mke wa Kanali Gaddafi na watoto wake watatu kukimbilia nchi
jirani ya Algeria. Algeria imejitetea kwa hatua hiyo waliochukua, huku
waasi wakiita " kitendo cha kiburi". Mpaka sasa mahala alipo Kanali
Gaddafi haijulikani. Wakati huo huo huo huko Libya, waasi wanajaribu
kupambana na wanaomtii Gaddafi, na kujiandaa kusogea Sirte.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)