Rais
Dk.Jakaya Kikwete akipata maelezo kutoka kwa Meneja mawasiliano wa
Vodacom Tanzania Bw Salum Mwalim jinsi ambavyo Vodacom inavyochangia
maedeleo ya vijijini kupitia teknolojia ya simu ya mkononi ikiwemo
huduma ya m-pesa na MWEI huku akipitia jarida la Vodacom alipotembelea
banda la kampuni hiyo katika maonesho ya wadau wa mawasiliano ya simu
yanayofanyika sanjari na mkutano mkuu wa mwaka wa wadau wa sekta ya
mawasiliano barani Afrika - CTO. jijini Dar es salaam ambao Vodacom ni
mdhamini.
Rais
Dk. Jakaya Kikwete akioneshwa na Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania
Bw. Salum Mwalim fulana ya Vodacom yenye logo na rangi mpya za kampuni
hiyo tangu ilipobadilika kutoka buluu kuwa nyekundu Aprili Mwaka huu
wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maoensho ya sekta ya
mawasiliano yanayofanyika sanjari na mkutano wa mwaka wa wadau wa
mawasiliano ya simu barani Afrika jijini Dar es salaam jana ambao
Vodacom ni mdhamini.
Mkuu
wa Huduma za kifedha wa kampuni ya Vodacom Jacques Voogtz akiwasilisha
mada juu ya njia za kusaidia maendeleo vijijini kupitia teknolojia za
mawasiliano ya simu katika mkutano wa mwaka wa taasisi ya mawasiliano
ya Jumuiya ya Madola - CTO unaofanyika jijini Dar es salaam. huduma ya
m-pesa imekuwa mfano mzuri wa ukombozi wa kimawasiliano katika nyanja
ya kifedha kwa wananchi vijijini hapa nchini.
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Bw.
Salum Mwalim (kulia)akitoa maelezo kwa Meneja Mwandamizi wa Programu
wa Taasisi ya mawasiliano ya jumuiya ya Madola - CTO Lesantha De Alwis
kupitia huduma za m pesa
na MWEI katika banda la Vodacom kwenye maonesho ya wadau wa
mawasiliano Afrika yanayoendelea jijini dar es salaam sanjari na
mkutano mkuu wa mwaka wa CTO.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)