Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen leo (Agosti 25 mwaka huu) ametangaza
kikosi cha wachezaji 23 kwa ajili ya mechi ya mchujo dhidi ya Algeria
‘Desert Warriors’ kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa
ya Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Equatorial Guinea na Gabon.
Wachezaji
walioitwa ni makipa Shabani Dihile (JKT Ruvu Stars), Juma Kaseja
(Simba) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni nahodha Shadrack
Nsajigwa (Yanga), Idrissa Rajab (Sofapaka, Kenya) na Amir Maftah
(Simba). Mabeki wa kati ni Aggrey Morris (Azam), Juma Nyoso (Simba) na
Victor Costa (Simba).
Viungo
wakabaji ni Henry Joseph (Kongsvinger IL, Norway), Nurdin Bakari
(Yanga), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Juma Seif (Yanga) na Jabir Aziz
(Azam). Viungo washambuliaji ni Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps,
Canada), Mrisho Ngassa (Azam) na Salum Machaku (Simba).
Washambuliaji
ni Abdi Kassim (DT Long An, Vietnam), Mbwana Samata (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Ramadhan Chombo (Azam), Dan
Mrwanda (DT Long An, Vietnam), Athuman Machupa (Vasalund IF, Sweden) na
John Bocco (Azam).
Timu
itaingia kambini Jumapili (Agosti 28 mwaka huu) mchana na jioni
itaanza mazoezi kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Mechi dhidi ya
Algeria itachezwa Septemba 3 mwaka huu kuanzia saa 10.00 jioni kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)