Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
DAR ES SALAAM
Mazungumzo
bado yanaendelea kati ya Serikali na Muwekezaji aliyejitokeza
kununua jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo katika makutano ya
barabara ya Kivukoni na Ohio jijini Dar es Salaam.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Celina Kombani wakati
akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya
makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.
“Kuhusu
suala la uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani, mazungumzo baina ya
Serikali na muwekezaji aliyejitokeza bado yanaendelea hivyo basi
napenda kuwatoa hofu waheshimiwa wabunge kuhusiana na suala hili,”
amesema waziri Kombani.
Waziri
Kombani amefafanua kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya muwekezaji
na ofisi mbalimbali za Serikali kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Mahakama ya Rufani,Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya
Katiba na Sheria na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aidha,
Waziri Kombani amesema muwekezaji aliyejitokeza ameahidi kujenga
mahakama ya Rufani yenye hadhi kulingana na umuhimu waka kama mhimili
mojawapo wa dola.
Kama
muafaka utafikiwa kati ya muwekezaji na Serikali jengo hilo la
Mahakama ya Rufani litajengwa maeneo ya mtaa wa Chimala mkabala na
barabara ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Hivi
karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitoa taarifa
kuhusiana na jengo la Mahakama ya Rufani kununuliwa na muwekezaji wa
hoteli ya Kempinski na kuwa sehemu ya hoteli hiyo kwa ajili ya maegesho
ya magari.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)