Ofisa
Mkuu wa Fedha wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Mrisho Shaban
(kushoto) akimkabidhi msaada wa vyakula Mwalimu Mkuu Msaidizi wa shule
ya msingi Uhuru Mchanganyiko, Juma Lukinga kwa ajili ya sikukuu ys Eid
El Fitr wanafunzi wenye ulemavu wanaosoma katika shule hiyo. Hafla hiyo
ilifanyika jijini Dar es Salaam leo.
Na Francis Dande
KAMPUNI ya simu Tanzania (TTCL) leo
imetoa msaada wa vyakula kwa watoto walemavu wa shule ya Uhuru
mchanganyiko pamoja na wasiojiweza katika kituo cha SOS kilichopo Mwenge
jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi misaada
hiyo vyenye thamani ya shilingi mil 3.5. ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni
hiyo Mrisho Shaaban alissema msaada huo unalenga kusherehekea sikukuu
ya Idd Elfitr pamoja na watoto ambao kwa namna moja ama nyingine ni
kundi linalohitaji kusaidiwa na jamii inayoizunguka.
“Sisi TTCL kama
kampuni ya umma na ya kizalendo tunajali sana jamii inayotuzunguka
pamoja na matatizo yake ndio maana leo tunatoa msaada wa vyakula kwa
makundi haya ya watoto wahitaji kwa kuwa in jukumu letu kama kammpuni ya
kitanzania kusaidia,”alisema Shaaban.
Alisema mbali na
kutoa misaada kwa Uhuru na SOS lakini pia tayari wametoa misaada kama
hiyo kwa vikundi vya wazee , yatima na walemavu wa viungo vya mwili
mjini Moshi ambapo vikundi vitatu kila kimoja kilipatiwa vyakula vyenye
thamani ya shilingi milioni moja na laki tano.
“Tunaahidi kuendelea
kuhudumia jamii yetu pale kampuni inapofanya vizuri na mapato
kuongezeka kwani ndio njia mojawapo ya kurudisha baadhi ya mapato
tuliyokusanya kwa wateja wetu ,”alisema Shaaban.
Aidha aliwaomba
watanzania kuendeleza ushirikiano na kampuni hiyo katika kupinga hujuma
zozote dhidi ya mtandao na kampuni ya TTCL kwa ujumla.
Naye mwalimu mkuu
msaidizi wa shule hiyo Juma Lukinga alisema sio mara ya kwanza kupokea
misaada mbalimbali kutoka kwa TTCL na kwamba anamshukuru mungu kwa kuwa
misaada hiyo inawasaidia sana kutokana na hali ngumu ya maisha iliyopo.
Alisema misaada hiyo
itawasiaida kula na watoto katika sikukuu ya Idd na kwamba watajiona
wanafuraha sawa na watoto wengine .
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)