Mwenyekiti wa Taifa-Chadema,Mheshimiwa Freeman Mbowe
--
CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA).
TAARIFA KUHUSU MAAMUZI YA KAMATI KUU YA CHADEMA
YALIYOFIKIWA KATIKA MKUTANO WA DHARURA ULIOFANYIKA SIKU YA
JUMAMOSI/JUMAPILI TAREHE 06-07 AGOSTI 2011 KATIKA HOTELI YA IMAGI MJINI
DODOMA.
Kamati
Kuu ya CHADEMA ilikutana katika Mkutano wa Dharura uliofanyika siku ya
Jumamosi na Jumapili tarehe 06 Agosti 2011 katika Hoteli ya Imagi Mjini
Dodoma. Pamoja na mambo mengine Ilifikia maamuzi yafuatayo :
1. Kamati Kuu ilipokea taarifa ya utekelezaji wa maagizo
iliyoyatoa katika Mkutano wake wa tarehe 17 Julai 2011 iliyowataka
madiwani wa CHADEMA Arusha kujiuzulu nafasi walizozipata pamoja na
kuomba radhi kwa makosa waliyoyafanya kutokana na mwafaka uliofikiwa
baina yao na madiwani wenzao wa TLP na CCM kwa kuwa chama hakikuridhia
wala kuutambua mwafaka huo.
2. Kamati Kuu imezingatia kuwa, kati ya madiwani 10 waliopewa
maelekezo na Kamati Kuu, madiwani watano (5) ndio wametekeleza maelekezo
kikamilifu wakati madiwani wengine watano (5) wamekataa kuyatekeleza
maelekezo hayo.
3. Baada ya kutafakari kwa kina taarifa ya utekelezaji wa maagizo
ya Kamati Kuu, na kuwapa nafasi ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu
Madiwani ambao walikuwa hawajatekeleza maelekezo,Kamati Kuu imezingatia
kuwa madiwani wamekataa kutekeleza maagizo ya Kamati Kuu.
Aidha, Kamati Kuu imezingatia kuwa kitendo cha madiwani kukataa
kutekeleza maagizo halali ya Kamati Kuu ni utovu mkubwa wa nidhamu na ni
kuvunja maadili na kanuni za chama, na kinaenda kinyume na msingi mama
wa CHADEMA wa uwajibikaji.
Hivyo basi, kwa kutumia mamlaka ya Kikatiba Kamati Kuu imewafukuza
uanachama madiwani watano wafuatao kwa kosa la kukataa kutekeleza
maagizo ya Kamati Kuu:
i) Ndugu Estomih Mallah
ii) Ndugu John Bayo
iii) Ndugu Charles Mpanda
iv) Ndugu Rehema Mohamed
ii) Ndugu John Bayo
iii) Ndugu Charles Mpanda
iv) Ndugu Rehema Mohamed
v) Ndugu Reuben NgowiWatajwa
hapo juu wamejulishwa maamuzi ya Kamati Kuu ndani ya Mkutano tarehe 07
Agosti 2011 saa 7:57 usiku, Aidha, kila mmoja wao atakabidhiwa barua
yenye kueleza maamuzi ya Kamati Kuu.
4.
Aidha, Kamati Kuu imepokea taarifa ya mazungumzo baina ya
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, na Waziri Mkuu, Mhe
Mizengo Pinda, juu ya nia na azima ya kumaliza tatizo la mgogoro wa
umeya Arusha, waliyoyafanya asubuhi ya siku ya Jumamosi, Tarehe 06
Agosti 2011 nyumbani kwa Waziri Mkuu Mjini Dodoma.
Kamati imezingatia kuwa:
a.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Waziri Mkuu wamekubaliana kuunda
Kamati ya Kitaifa ya kushughulikia mgogoro wa umeya wa Arusha
itakayojumuisha wajumbe kutoka sehemu mbili zinazohusika katika mgogoro
huu ambazo ni CCM na CHADEMA
b.
Kamati ya Kitaifa ya Maridhiano itaundwa haraka iwezekanavyo, na
kwa vyovyote mgogoro wa u meya Manispa ya Arusha ulikubalika uishe ndani
ya mwezi mmoja tangu tarehe ya mazungumzo ya Mwenyekiti wa Taifa na
Waziri Mkuu
c. Uenyekiti wa Kamati ya Kitaifa utakuwa chini ya Msajili wa Vyama
vya Siasa, Ndugu John Tendwa, na kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa
ataratibu uundwaji wa Kamati hiyo ya Kitaifa.
5. Kamati Kuu imetambua juhudi za Waheshimiwa Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Mhe Freeman Mbowe, kwa
hatua yao chanya ya kumaliza mgogoro wa Arusha.
6. Pamoja na hatua njema kuelekea kumaliza mgogoro wa umeya
Arusha, Kamati Kuu ya CHADEMA itaendelea kusitisha kumtambua rasmi Meya
wa Arusha hadi pale mazungumzo yaliyoanishwa hapo juu yatakapokamilika
na mwafaka bayana kupatikana.
Imetolewa na:
……………….
Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
……………….
Mhe. Freeman Aikaeli Mbowe (Mb)
MWENYEKITI WA TAIFA-CHADEMA
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)