Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo (kushoto)
akizungumza na waandishi wa habari (leo) jijini Dar es salaam mara
baada ya kusaini msaada wa shilingi bilioni 40 kwa ajili ya miradi
miwili ya maendeleo. Mradi wa kwanza ni ujenzi wa daraja la Rusumo
lilopo mpakani wa Tanzania na Rwanda na uimarishaji wa barabara jijini
Dar es salaam. kulia ni Balozi wa Japan nchini Hiroshi Nakagawa.Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es
salaam
--
Na Hadija
Chumu na Moshi Stewart-Maelezo,Dar es Salaam
Serikali imesaini msaada wa shilingi
bilioni 40 na serikali ya Japan kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa miradi
miwili ya maendeleo hapa nchini.
Akiongea na wanahabari leo Waziri wa
Fedha na Uchumi Mustapha Mkulo amesema miradi hiyo ni ya ujenzi la wa
daraja la Rusumo litakalounganisha nchi ya Tanzania na Rwanda na
upanuzi wa barabara ya Kilwa ambapo itasaidia shughuli za maendeleo
baina ya nchi hizo.
Waziri
Mkulo alisema
Alisema
upanuzi wa barabara ya kilwa utapunguza kwa kiasi kikubwa
foleni na adha nyingine za kimiundombinu ndaji ya jiji la Dar es
salaam,
Nae Balozi wa Japani nchini Bw Hiroshi
Nakagawa amesema msaada huo ni matokeo ya ushirikiano
uliopo kati ya Japani na Tanzania ambapo utasaidia kuimarisha uchukuzi
na usafirishaji nchini,
Balozi
Nakagawa alisema kiasi cha bilioni 1.86 za kijapani zitasaidia upanuzi
wa daraja la Rusumo, wakati Yen Milioni 37 zimetolewa kukamilisha
upanuzi wa barabara ya kilwa
Nae mwakilishi
wa shirika la JICA nchini Bw Yukihide Katsuta amesema fedha
zilizotolewa na shirika hilo ni milioni 769 za kitanzania
ambazo zitasaidia kupata mwongozo sahihi wa kitaalam
utakaopelekea ubora katika ujenzi na upanuzi wa barabara ya kilwa
unaotegemea kukamilika hivi karibuni
Aidha
mwakilishi wa TANROADS Mhandisi Mfugale amesema watahakikisha mradi huo
unatekelezwa kwa wakati na ubora unaohitajika ili kuhakikisha na
kusimamia upanuzi wa daraja hilo pamoja na ule wa upanuzi wa barabara ya
kilwa unatimizwa kulingana na fedha zinazotolewa.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)