Home
Unlabelled
Mitambo ya Umeme ya Aggreko Yawasili Nchini
Mitambo ya Umeme ya Aggreko Yawasili Nchini
Mitambo ya Aggreko ikishushwa, tayari kwa kufungwa.
Sehemu
ya mitambo ya umeme ya Aggreko ikishushwa Ubungo jijini Dar es Salaam
tayari kuanza kufungwa na umeme wake kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa.
Moja ya kontena lenye mitambo ya Aggreco likiwasili leo mchana ubungo jijini Dar es Salaam
Meneja
wa Mahusiano wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Badra Masood,
akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye mitambo ya kufua
umeme, Ubungo jijini Dar es Salaam. Badra alisema kuwa magao wa umeme
utakoma kufikia mwezi Disemba mwaka huu. Akielezea mikakati mbali mbali
ambayo TANESCO imefanya ni alisema kuwa ni pamoja na kukodisha mitambo
yenye uwezo w kuzalisha Megawati 100, kutoka Kampuni ya Aggreco ya
Mombasa, Kenya. Mitambo iliyowasili leo na kazi ya kuifunga itatarajiwa
kuanza hivi hivi karibuni. Akielezea zaidi kuhusu ujio wa mitambo hiyo
ya Aggreco, Badra alisema kuwa hii ilikuwa ahadi ya Waziri wa Nishati
na Madini, William Ngeleja, alipokuwa akiwasilisha bajei ya wizara yake
Bungeni hivi karibuni. Mipango mingine ya kumaliza mgao wa umeme
ifikapo Disemba mwaka huu ni pamoja na kutumia mitambo ya Symbion yenye
uwezo wa kuzalisha Megawati 112, na mitambo ya Jacobsen inayoendelea
kufungwa hatua inayoipa Tanesco uhakika wa kumaliza kero ya mgao wa
umeme mwezi Disemba mwaka huu.Picha na Victor Makinda
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)
Lukaza Blog is a resources blog providing high quality articles with premium topics and well drafted. The main mission of Lukaza Blog is to provide the best quality articles which are relevance, original, truth and education materials designed and perfectlly to deliver best result for your knowledge and understanding of new things.
Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Mzee Emannuel Humba akionyesha tuzo yake aliyopewa na mfuko huo kwa kutambua...
Contact Form
About Me
Hello, my name is Josephat Lukaza. I've 12 years in Blogging and An Award Winner for the BEST Political Blog in African Bloggers Awards in 2015 Learn More →
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)