Mke
wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA ) Mama Salma Kikwete akisoma nakala ya RAPID WOMEN Model ambayo
ni kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga
mwanamke, matumizi ya kielelezo hicho yanalenga zaidi wanawake viongozi
katika kuhamasisha jamii. Muundo huo wa kitendea kazi uliwasilishwa na
Dr. Sara Clark (hayupo pichani) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Futures Group International leo katika ofisi za WAMA zilizopo
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dr.
Sara Clark (kushoto) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Futures Group International akimuonyesha Mke wa Rais ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA ) Mama Salma
Kikwete (kulia) mfuko wa kuwekea vitu mbalimbali ambayo inatumika kama
matangazo inayotengenezwa na kampuni hiyo wakati alipomtembelea
ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuwasilisha
muundo wa kitendea kazi cha utetezi wa uzazi wa mpango na afya
zinazomlenga mwanamke.
Mke
wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo
(WAMA) (katikati) Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Dr.
Sara Clark (kushoto) ambaye ni Makamu Rais na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Futures Group International na Millicent Obayo ambaye ni Mkurugenzi
Mkazi wa kampuni hiyo wakati walipomtembelea ofisini kwake Ikulu jijini
Dar es Salaam leo kwa ajili ya kuwasilisha muundo wa kitendea kazi cha
utetezi wa uzazi wa mpango na afya zinazomlenga mwanamke.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)