Mbunge
wa Singida Mjini Mh. Mohammed Dewji akiwa Bungeni huku akibadilishana
mawazo na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Lucy Nkya.
----
----
Na.Mwandishi wetu.
Mbunge
wa Jimbo la Singida Mjini, Mohammed Dewji, ametoa ufafanuzi juu ya
tuhuma zilizotolewa na baadhi ya wakazi wa Singida za kwamba hajafanya
chochote cha maendeleo katika jimbo lake tangu kuchaguliwa kwake .
Tuhuma
na malalamiko hayo yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wa Singida
kupitia mtandao wa kijamii wa FACEBOOK, wakati wa kubadilishana mawazo
na Mbunge huyo.
Wananchi
hao ambao waliruhusiwa kutoa maoni na dukuduku zao kwa mheshimiwa
DEWJI walidai kutoona maendeleo yoyote katika jimbo hilo kwa madai
kwamba wananchi wa SINGIDA wamekuwa wakiteseka na maisha kwa kukosa
maji, ajira na masuala ya maendeleo.
Katika
ufafanuzi wake kuhusiana na Malalamiko hayo, Mheshimiwa Dewji amesema,
Tangu kuchaguliwa kwake amekuwa mstari wa mbele katika kuleta
mabadiliko ya kimaendeleo katika maeneo ya Kero za Maji ambapo
amefanikisha uchimbaji wa visima virefu zaidi ya 21, kwenye kata za
Unyambwa, Mungu Maji, Unyamikumbi, Mwankoko, Mtamaa, Mandewa na Mtipa
pamoja na baadhi ya kata za Mjini Kama Kindai, Mitunduruni na Utemini.
Aidha
Mheshimiwa Dewji pia ameongeza kuwa bado anaendelea na jitihada za
kukabiliana na tatizo hilo kwa kuibana Serikali itekeleze mradi Mkubwa
wa Benki ya Dunia wa kuchimba visima 10 jimboni na anaendelea kuibana
Serikali ifanye haraka kumalizia mradi mkubwa mwingine wa maji
unaofadhiliwa na Benki ya BADEA na OPEC .
“Mradi
huo ukikamilika ndio utakuwa ufumbuzi wa tatizo la maji katika
manispaa ya Singida. Mradi huu utabadilisha miundombinu yote ya Maji
safi ndani ya manispa yetu. Mradi huu unatarajia kukamilika 2013 na
utagharimu takriban billion 20”.Amesema Mheshimiwa Mbunge Dewji.
Kuhusu
ajira DEWJI ameeleza kuwa amekuwa mstari wa mbele katika kutoa Ajira
kwa vijana kupitia kampuni yake ya Mohamed Enterprises Limited(MeTL)
sambamba na makampuni mengine mbalimbali.
Amefafanua
zaidi kuwa yuko mbioni kuwekeza katika jimbo lake kwa kufungua kiwanda
kitakachotoa fursa zaidi kwa vijana na wakazi wa Singida kujipatia
maendeleo na ajira, na kwamba kwasasa anaendelea kuwasiliana na
wataalamu mbalimbali wa uwekezaji ili kuona kama kuna fursa za kuweza
kuwekeza katika manispaa ya hiyo.
Amepongeza
kupokelewa kwa wito wa kuhamasisha michezo katika Jimbo lake na
kusisitiza kuwa ataendelea kunyanyua na kuibua vipaji kupitia
mashindano yake yajulikanayo kama Mohammed Dewji Cup yakiwa na takribani
miaka SABA na yamekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana wazaliwa wa
Singida.
“Kuhusiana na Suala la Ujenzi wa Uwanja wa Namfua nilishaanza ukarabati
katika eneo la Jukwaa kuu wewe mwenyewe ni shahidi kama ulikuwa
unaufahamu uwanja ulivyokuwa mwanzo na wakati wa mashindano ya riadha
Kitaifa niliweza kukarabati eneo la kukimbilia wanariadha na bado
nitaendelea kukarabati kwa awamu mpaka tutakapoukamilisha. Ukumbuke
ahadi hii haikuwa yangu peke yangu. Ila nimeshanunua nyasi za bandia
ambazo zimenigharimu million 250. Natarajia kuziweka hizo nyasi
2012/13.”
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)