
Mwakilishi
Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alberic Kacou akifungua
rasmi semina ya waandishi wa habari na wataalamu mbalimbali wa
mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania nchini, juu ya mpango kazi
maalum wa miaka minne unaojulikana kama United Nations
Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP) Semina imefanyika kwenye
Hoteli ya Movenpick jijini Dar es Salaam.

Mtaalamu
wa Masuala ya Kulinda Haki za Watoto wa UNICEF Mona Aika akitoa
maelekezo kwa Mwandishi wa habari wakati wa semina ya mpango kazi maalum
wa miaka minne unaojulikana kama United Nations
Development Assistance Plan 2011-2015 (UNDAP).
Mmoja
wa watumishi wa IAGG Bi. Salome Anyeti akitoa ufafanuzi kwa waandishi
wa habari juu ya masuala ya Haki na Jinsia katika mwendelezo wa semina
iliyoandaliwa na UN Tanzania kwa lengo la kuhamasisha waaandishi wa
habari kuandika na kuelimisha jamii juu ya mpango wa MKUKUTA na MKUZA
kwa kipindi cha miaka 4 ijayo. Kushoto ni Bw. Robert Basil Mwenyekiti
wa IAGG upande wa Jinsia na Maambukizo ya Ukimwi kutoka kitengo cha
Chakula na Kilimo UN.
Mratibu
wa Ukuaji Uchumi kutoka FAO Dkt. Vedasto Rutachokozibwa akibadilishana
mawazo na waandishi wa habari katika Semina ya UNDAP iliyofanyika
jijini Dar es Salaam.
Afisa
Uhusiano wa UNHCR Juliana Bwire akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu mpango mzima wa UNDAP kwa upande wa sekta ya wakimbizi ambayo
Mwakilishi Mkazi wa UN nchini Alberic Kacou amesisitiza ushirikiano wa
pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Afisa
Program wa WFP Said Johari na Afisa Uhusiano wa michango wa WFP Fizza
Moloo wakizungumza na mwandishi wa habari alitembelea kitengo hicho
wakati wa semina ya mpango kazi maalum wa miaka minne unaojulikana kama
United Nations Development Assitance Plan 2011-2015 (UNDAP).





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)