Baadhi ya Warembo wa
Vodacom Miss Higher learning waliokuwa katika ziara ya kutembelea Makao
makuu ya Vodacom Tanzania yaliyopo Mlimani City jijini Dar es salaam
ambapo shindano lao linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki mjini
Dodoma.
Mmoja wa warembo wa
Vodacom Miss Higherlearning akimuualiza Meneja wa Vodashop Mlimani City
Bi. Fatma Kalyanye swali juu ya huduma zinazoedeshwa na vodashop pindi
walipozuru Makao makuu ya Kampuni hiyo jana.
Meneja wa Vodashop Mlimani
city Fatma Kalyanye akiwaelekeza warembo wa Vodacom Miss higher
learning waliozuru duka hilo namna ya kuweka nyaraka za kudumu za wateja
wao wa M pesa,warembo hao walitembelea makao makuu ya kampuni hiyo
ikiwa ni moja ya hatua za kuelekea kilele cha shindano lao
liatakalofanyika mwishoni mwa wiki mjini dodoma.
Mfanyakazi wa Vodacom
Tanzania kitengo cha huduma kwa wateja Bw. Hiramu Mungai akitoa
ufafanuzi wa jinsi ya kutoa huduma kwa wateja kwa Warembo wa Vodacom
Miss higherlearning waliokuwa katika ziara ya kutembelea makao makuu ya
kampuni hiyo jana.
Mfanyakazi wa Vodashop
Mlimani City Jane Mrosso Akiwapa maelekezo ya matumizi ya simu
mbalimbali baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Higher learning
walipotembelea duka hilo hapo jana,ikiwa ni hatua mojawapo ya kuelekea
katika shindano lao linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki mjini
Dodoma.
Mkuu wa kitengo cha huduma
kwa wateja wa Vodacom Tanzania Najenjwa Mbaga akisalimiana na warembo
wa Vodacom miss higherlearning walipozuru makao makuu ya kampuni hiyo
jana wakiwa safarini kuelekea mjini Dodoma katika fainali za shindano
lao litakalofanyika mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya Warembo wa
Vodacom Miss Higher learning wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya
kumaliza ziara yao ya kutembelea Makao makuu ya Vodacom Tanzania
yaliyopo Mlimani City jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)