Mkurugenzi wa Dar Metropolitan
Promotions ambao ni waandaaji Mashindano ya Redd's Miss Ilala,Jackson
Kalikumtima (katikati) akionge na waandishi wa Habari (hawapo pichani)
leo wakati wa kutangaza rasmi kambi ya Redd's Miss Ilala 2011 katika
hoteli ya Lamada,Ilala jijini Dar es Salaam.Kulia ni Ofisa Udhamini wa
Vodacom Tanzania,Ibrahim Kaude na kushoto ni Jesse Jackson wa
Dar Metropolitan Promotions
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL),Fimbo Buttallah (kushoto) akiongea na Warembo
wanatakaoshiriki katika Mashindano ya Redd's Miss Ilala 2011 (hawapo
pichani).
Miss Ilala 2010,Bahati Chande akiongea
na Waandishi wa Habari.
Kikao cha Uongozi wa Redd's Miss Ilala
2011 na warembo washiriki kikiendelea katika hoteli ya Lamada,Ilala
jijini Dar.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia
Tanzania (TBL),Fimbo Buttallah (pili kulia) akipena mkono na Warembo
watakaoshiriki mashindano ya Redd's Miss Ilala 2011 na kuwatakia kila la
kheri katika kambi yao inayoanza leo kwenye hoteli ya Lamada,Ilala
jijini Dar.kulia ni Mrembo anaemaliza muda wake,Bahati Chande.
Mtaalam wa Mambo ya Habari wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu akipena mkono na Warembo watakaoshiriki
mashindano ya Redd's Miss Ilala 2011.Kulia ni Msimamizi wa Warembo
hao,Sylvia Shally.
Warembo wakiwa katika picha ya pamoja
na Wasimamizi wao.
Baadhi ya Wanahabari wakiwajibika.
Warembo woote katika picha ya pamoja.
WAREMBO 21 wameanza kambi ya Reds
Miss Ilala ilioanza jana katika hoteli ya Lamada, Dar es salaam.
Katika
kambi hiyo warembo hao walianza kwa semina ya siku moja ambapo
walielekezwa masuala mbalimbali muhimu ya kijamii.
Akizungumza
katika semina hiyo mratibu wa Miss Ilala Jackson Kalikumtima aliwataka
warembo hao kuwa makini na watu wanaoweza kuwaharibia sifa zao za
kushiirki shindano hilo.
Alisema
kuwa warembo wengine hushindwa kumaliza shindano hilo kutokana na
kujikuta wakiwa katika kashfa na vitendo vuisivyokuwa na maadili.
Naye
Meneja Masoko wa kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah aliwataka
warembo hao kujitambua na kuwa mstari wa mbele katika kuonesha maadili
mema.
Alisema
kuwa TBL kupitia kinywaji cha Reds imeamua kudhamini kanda tatu za Dar
es salaam ambazo ni Ilala, Kinondoni na Temeke na kwa sasa mashindano
hayo yatakuwa yakiitwa Reds Miss Ilala, Kinondoni au Temeke.
“ Ni
kwamba kama ambavyo Reds ilivyo karibu na warembo au niseme akina dada
kiujumla na ndivyo ambavyo naona kuwa hata ninyi mnatakiwa kuwa karibu
na jamii na kuwa mfano katika jamii inayowazunguka” alisema Butallah.
Warembo
hao ni Jenifer Kakolaki, Alexia William ,
Meryvine Kenzia, Patricia Kajubi,
Salha Israel, Lilian Paul, Diana
John’ Judith Mlingwa, Nasra
Salim’ Cresencia Haule,Godliver
Mwashamba, Williet Wilson,Faizal Ally, Priscilla Mchemwa,
AugostinaMshanga, Ritha Cuthbert , Lilian Bryceson,
Maria John, Lilian William, Edna Mnada,Mariam
Manyanya.
Shindano
hilo litafanyika Julai 29 (siku ya Vunja jungu) katika ukumbi ulioko
katikati ya jiji la Dar es salam.
Wadhamini waliojitokeza kudhamini Shindano hilo
ni Redds Original inayozalishwa na kiwanda cha Tanzania Breweries
Limited ambao ndio wadhamini wakuu, wengine ni Vodacom Tanzania,
Tanzania Standard Newspapers, Fabak Fashion, TV Sibuka, Maisha Club, na
88.4 Clouds FM na Paris Pub ya Tabata.
“
Watakapokuwa kambini warembo watajifunza mambo mbali mbali yanayohusu
mashindano ya urembo, mambo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kibiashara.
Pia watajifunza namna ya kujitunza kama wasichana na kufanya shughuli
za kijamii.” Alisema Kalikumtima
Kwa Hisani Ya Michuzi Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)