TIMU ya
taifa ya soka ya wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’ ilianza vema michuano
ya Shirikisho la Soka Kusini mwa Afrika (COSAFA) kwa kuichapa mabao
3-1 Botswana kwenye Uwanja wa Gwanzura jijini Harare, Zimbabwe.
Katika
mechi hiyo iliyokuwa ya kuvutia walioing’arisha ni Mwanahamis Omar
‘Gaucho’ aliyetupia nyavuni mabao mawili dakika ya tisa na 88 huku
Fatuma Mustafa ‘Kitu Nini’ dakika ya 32.
Twiga
iliyo kundi A katika michuano hiyo, kesho itaivaa Lesotho kwenye Uwanja
wa Rufaro kabla ya kumaliza mechi za makundi Julai 5 dhidi ya wenyeji
kwenye Uwanja wa Gwanzura.
Hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo
itafanyika Julai 7, ambako kila kundi litatoa timu mbili kuingia katika
hatua hiyo.
Twiga Stars inashiriki michuano hiyo kama
mwalikwa, ambapo timu nane zinatarajiwa kushiriki, ambazo ni Zimbabwe,
Lesotho, Botswana, Afrika Kusini, Zambia, Msumbiji na Malawi.
Habari kwa
hisani ya Francis Godwin
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)