Taswira Za Maonyesho Ya Kwenye Banda La Wizara Ya Nishati Na Madini Mjini Dodoma - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

Taswira Za Maonyesho Ya Kwenye Banda La Wizara Ya Nishati Na Madini Mjini Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akipata maelezo ikiwa ni pamoja na kuoneshwa juu ya shughuli za upimaji wa mafuta ya magari unavyofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) alipotembelea banda hilo kwenye maonesho hayo.Anayetoa maelezo ni Mhandisi Melania Kamugisha ambaye ni mtaalamu wa mamlaka hiyo.
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (CCM) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa mradi wa Biofueli, Ester Mfugale alipotembelea jana banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonesho yake yanayoendelea kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Gregory Teu, akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Assa Mwakilembe juu ya shughuli zinazofanywa na Wizara hiyo mara alipotembelea banda hilo jana.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Gregory Teu, akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Arti Tanzania Limited inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Abdalah Seushi juu ya shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo mara alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma.
Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini, Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika (CHADEMA) akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA),Paul Masanja alipotembelea banda hilo ili kupata maelezo juu ya shughuli za ukaguzi wa madini zinazofanywa na Wakala huo.Picha Zote na Mdau Greyson Mwase

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages