Upangaji
makundi ya mechi za mchujo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2014
nchini Brazil ulifanywa jana (Julai 30 mwaka huu) karibu na ufukwe wa
Copacabana jijini Rio de Janeiro nchini Brazil ukiongozwa na Katibu
Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) Jerome Valcke.
Taarifa
iliyotolewa na msemaji wa shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF)
Bw. Boniface Wambura imesema, Timu ya Tanzania (Taifa Stars) imepangwa
kundi C Kanda ya Afrika ambalo lina timu za Cote d’Ivoire, Morocco na
Gambia. Lakini kabla ya kuingia katika kundi hilo Stars italazimika
kucheza raundi ya kwanza ya mchujo dhidi ya Chad.
Stars ikifanikiwa kuitoa Chad baada ya mechi mbili za nyumbani na ugenini zitakazochezwa kati ya Novemba 11-15 mwaka
huu ndiyo itaingia katika kundi hilo la C. Pia mshindi wa kundi C ndiye
atakayeingia katika raundi inayofuata kabla ya kupata tiketi ya kwenda
Brazil.
Stars
ni miongoni mwa timu 29 ambazo kwenye viwango vya ubora vya FIFA vya
Julai mwaka huu katika Afrika ziko chini ya timu 24 bora, hivyo
kulazimika kuanzia hatua hiyo ya kuchujana zenyewe kabla ya kuingia
hatua ya makundi ambayo itachezwa kuanzia Juni 1, 2012 hadi Septemba
10, 2013.
Kwa
mujibu wa viwango vya FIFA vya Julai mwaka huu, Tanzania iko katika
nafasi ya 127 wakati Chad ni namba 158. Kwa upande wa Afrika, Tanzania
ni namba 33 na Chad 43. Nchi 52 kati ya 53 za Afrika zimeingia katika
michuano hiyo ya Kombe la Dunia. Ni Mauritania pekee ambayo
haikuthibitisha ushiriki wake.
Timu
10 za juu kwa ubora barani Afrika ambazo zimeongoza makundi 10 ya
Afrika katika upangaji ratiba ni Afrika Kusini, Tunisia, Cote d’Ivoire,
Ghana, Burkina Faso, Nigeria, Misri, Algeria, Cameroon na Senegal.
Afrika ina nafasi tano kwenye fainali za Kombe la Dunia, huku Ulaya ikiongoza kwa kuwa nazo 13.
Habari Kwa Hisani Ya John Bukuku - Full Shangwe Blogu
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)