Raisi Jakaya Kikwete Na Mkewe Mama Salma Wakipita Mbele ya Jeneza Wakitoa Heshima Za Mwisho
Rais
Dr. Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la kada wa CCM
na mpigania uhuru, mzee David Zimbihile wakati wa mazishi ya kada huyo
mkongwe (80) yaliyofanyika Muleba, Mkoani Kagera jana. Pichani juu:Mwenyekiti
wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete
wakitoa heshima za mwisho kwa marehemu mzee David Zimbihile wakati wa
ibada ya mazishi iliyofanyika Muleba jana jioni. Mzee Zimbihile
aliyewahi kuwa mbunge na kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama Cha
Mapinduzi alizikwa kwa heshima zote kijijini mwake Muleba, mkoani
Kagera.
Mwenyekiti
wa CCM, Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete
wakiweka shada la maua katika kaburi la mpigania uhuru na kada mkongwe
wa CCM, David Zimbihile wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Muleba,
mkoani Kagera jana jioni. Marehemu Zimbihile alianza harakati za
ukombozi wa mwafrika nchini Kongo (DRC) ambapo alifanya kazi kwa karibu
na Marehemu Patrice Lumumba na baadaye kupitia vyama vya wafanyakazi
alikutana na Marehemu Kwame Nkurumah na hatimaye alirejea nchini
Tanzania kuendelea na harakati hizo.
Picha na Freddy Maro





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)