Nelly akiwasili Dar
Maria Sarungi Akimpokea Nelly
Mrembo
aliyeshinda taji la Miss Universe Tanzania 2011 Nelly Kamwelu ameshinda
taji la Miss Southern Afrika International 2011 katika mashindano
yaliyofanyika Ndola nchini Zambia na kushirikisha warembo kutoka nchi
mbalimbali za kusini na mashariki mwa Afrika.
Nelly
aliyepata mwaliko wa kushiriki mashindano hayo kupitia bodi ya Utalii
Tanzania (TTB) ameshinda taji hilo jumapili ya Juni 27 mwaka huu. Fursa
hiyo imemsaidia Nelly kupata uzoefu kabla ya kwenda katika mashindano ya
Miss Universe kimataifa mwezi wa nane na tisa mwaka huu.
Mashindano
hayo mbali ya kujenga mshikamano miongoni mwa nchi za kiafrika
yanalenga pia kuvutia na kutangaza utalii wa nchi washiriki.
Mbali
na kuhsiriki shindano la urembo,wakiwa nchini Zambia warembo washiriki
akiwemo Nelly walihsiriki na kufanya kazi mbalimbali za kijamii kama
vile kutembelea hospitali za watoto na vituo vya kulelea watoto na
kushiri maonyesho ya kimataifa ya biashara nchini humo.
Ukiondoa
Tanzania nchi nyingine za Afrika zilizoshiriki ni Namibia, Zambia,
Lesotho, Afrika ya Kusini, Botswana, Zimbabwe, Swaziland, Congo, Malawi
na Msumbiji.
Nyota
ya Nelly ilianza kung’ara pale aliposhinda taji la Miss Universe katika
shindano lililodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom
Tanzania ikiwa ni sehemu ya azma ya kampuni hiyo ya kuibua,kuendeleza na
kulinda vipaji vya vijana wa kitanzania katika sanaa na michezo.
Azma
hiyo inalenga kuwapatia fursa vijana ya kujiendeleza kimaisha kupitia
vipaji pamoja na kutimiza ndoto walizonazo katika sanaa.
Kwa
kushikilia taji la Miss Southern Afrika Internation Nelly anawajibu wa
kutoa elimu kwa jamii juu ya saratani ya matiti na mfuko wa uzazi na
atakuwa balozi wa nia njema wa mtandao wa saratani ya matiti na mfuko wa
uzazi Zambia.
Aidha
ushindi huo umempatia Nelly pamoja na zawadi mbalimbali mshahara wa
kwacha millioni moja kwa mwezi kwa kipindi cha miezi kumi na minne.
Source: Mbeya Yetu Blog |
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)