Mjumbe
katika ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Chama
cha wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) unaofanyika London Uingereza,
Mhe. Zito Kabwe akichangia hoja kuhusu msimamo wa Africa kwenye
maandalizi ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama hicho. Wabunge wa Afrika
katika Kikao chao hicho hawakufikia msimamo wa pamoja kuhusu Mgombea
watakayempendekeza mpaka watakapo kutana tena kesho. Jumla ya wagombea
watatu kutoka, Uingereza, Pakistani, na visiwa vya Samoa, wanawania kiti
hicho.
Ujumbe
wa Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Chama cha wabunge wa Jumuiya ya
Madola (CPA) unaofanyika London Uingereza, wakifuatilia kwa makini hoja
kutoka kwa wajumbe wanaowania uwenyekiti wa Dunia wa chama hicho. Kutoka
Kushoto Ni Ndg. Emmanuel Mpanda, anayemwakilisha katibu wa Bunge, Naibu
Spika Mhe. Job Ndugai, Mhe. Zungu, Mhe. Beatrice Shelukindo, Mhe. Zitto
Kabwe na Mhe. Maua Daftari. Jumla ya wagombea watatu kutoka, Uingereza,
Pakistani, na visiwa vya Samoa, wanawania kiti hicho. Picha na Owen
Mwandumbya wa Bunge
Mjumbe
katika ujumbe wa wabunge kutoka Tanzania katika Mkutano wa 57 wa Chama
cha wabunge wa Jumuiya ya Madola (CPA) unaofanyika London Uingereza,
Mhe. Zito Kabwe akiteta jambo na Mbunge Mwenzie kutoka Kenya mara baada
ya kikao cha kanda ya Afrika kumalizika. Kulia ni Spika wa Kenya Mhe.
Keneth Marende (Mb).
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)