MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGA MWILI WA MAREHEMU PROFESA MUSHI JANA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL AAGA MWILI WA MAREHEMU PROFESA MUSHI JANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya marehemu Profesa, Samuel Mushi, aliyefariki wiki iliyopita jijini Dar es Salaam. Shughuli za maziko na kuaga mwili wa marehemu zilifanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoa heshima ya mwisho mbele ya jeneza lenye mwili ya Marehemu Profesa Samuel Mushi, wakati alipofika katika shughuli ya kuaga iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwafariji wanafamilia ya marehemu Profesa Samuel Mushi, alipofika kuaga mwili katika Ukumbi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo Julai 27, 2011
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Waziri Mstaafu, Fredrick Sumaye, nje ya ukumbi wa Nkurumah baada ya kuaga mwili ya marehemu Profesa Samuel Mushi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, leo Julai 27, 2011. Katikati ni Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa.Baadhi ya wanafamilia ya marehemu Profesa Mushi, na ndugu jamaa na marafiki, wakiwa katika shughuli za mazishi na kuaga mwili wa marehemu Profesa Samuel Mushi, iliyofanyika leo Julai 27, 2011, kwenye ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages