Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu
Nyerere , Kivukoni na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salimu akizindua
maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho leo jijini Dar es salaam. Chuo hicho
kimeanzishwa tarehe 29 Julai mwaka 1961.Wageni wengine ni pamoja na Waziri Mkuu
Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba .
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akitoa
mada juu ya mchango wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika maendeleo
ya Taifa leo jijini Dar es salaam wakati wa uzindua maadhimisho ya miaka 50 ya
Chuo hicho . Chuo hicho kianzishwa tarehe 29 Julai mwaka 1961.
Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,
Kivukoni Dkt John Magotti akitoa hotuba ya ukaribisho leo jijini Dar es salaam
wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uanzishwaji wa Chuo
hicho.
Mawaziri Wakuu Wastaafu Jaji Joseph Sinde Warioba
(kushoto) na Dkt Salim Ahmed Salimu(kulia) wakibadilishana mawazo leo jijini Dar
e salaam wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50 ya uanzishwaji wa Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Kivukoni.
Wanajumuiya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,
Kivukoni wakicheza muziki leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa
maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo hicho .
Wanajumuiya wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ,
Kivukoni wakimsikiliza kwa makini hotuba ya uzinduzi wa maadhimisho ya miaka 50
ya Chuo hicho iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo
hicho na Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim(hayupo pichani).
Picha na Tiganya Vincent- MAELEZO- Dar es
salaam.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)