Waziri
wa Habari, Utalii,Utamaduni na Michezo, Abdilah Jihad (kushoto)akipokea
jezi kutoka kwa Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha GrandMalt,
Consolata Adam kwa ajili ya timu ya Baraza la Wawakilishi
Zanzibaritakayopambana na timu ya Klabu ya Wazee ya Arusha Septemba
8,mwaka huu. Anayeshuhudia katikati ni Makamu Mwenyekiti wa timu ya
Baraza, Mbarouk Mussa. Grand Malt ambayo imetoa vifaa hivyo vya michezo
vyenye thamani ya sh. milioni 10, ni wadhamini wa bonanza
italoshirikisha pia vilabu vingine vya veterani.
Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt, Consolata Adam(kulia)akihutubia katika hafla hiyo.
Waziri
wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo,Abdilah Jihad akitangaza rasmi
kuwa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt kimeruhusiwa kudhamini
michezo na shughuli mbalimbali kisiwani Zanzibar. Alitangaza
jana
mjini Zanzibar wakati Grand Malt ilipotoa vifaa vya michezo vyenye
thamani ya sh. milioni 10 kwa ajili ya bonanza la veterani
litakalofanyika Arusha Septemba 8, mwaka huu. Kulia ni Meneja wa
kinywaji hicho,
Consolata Adam na Makamu Mwenyekiti wa timu ya baraza, Mbarouk Mussa.
Waziri
wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad akiwa na baadhi ya
viatu walivyokabidhiwa.
Waziri
wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa
timu ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Abdilah Jihad (wa pili kushoto),
Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Mbarouk Mussa
(kushoto),
pamoja na Meneja wa kinywaji kisicho na kilevi cha Grand Malt,
Consolata Adam (kulia) wakigongeana kopo za kinywaji hicho wakati wa
hafla ya timu hiyo kukabidhiwa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh.
milioni 10, mjini Zanzibar jana.
wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Baraza la wawakilishi.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)