Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Songea, Ali Saidi Manya, Diwani wa kata ya
Lizaboni(Mwenye suti Nyeupe) amefariki dunia leo katika Hospitali ya
Misheni Peramiho.
Taarifa
za Msiba huo zimetangazwa na naibu Meya wa Manispaa ya Songea
Mheshimiwa Mariam Dizumba na kupokelewa kwa mshtuko mkubwa na wakazi wa
manispaa ya Songea Mkoa wa ruvuma kwa ujumla.
Naibu Meya Dizumba amesema mazishi ya Mstahiki Meya Ali Saidi Manya yatafanywa nyumbani kwake
Lizaboni Manispaa ya Songea Siku ya Jumatatu Tarehe 1 Agosti 2011.
Maandalizi yanaendelea na wageni kadhaa wa vyeo mbalimbali
wamethibitisha kuhudhuria.
Mtandao huu unaungana na familia katika kipindi hiki cha maombolezo. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahale pema peponi
Mtandao huu unaungana na familia katika kipindi hiki cha maombolezo. Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahale pema peponi
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)