Balozi
wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akiwasili katika Banda la
Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa ajili ya kuangalia na kujifunza
shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na shirika hilo katika kuwaletea
wananchi maendeleo.
Balozi
wa Ireland nchini Loccam Fullam(kulia) akikaribishwa na Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Neema Mbuja (kushoto)
jana jijini Dar es salaam wakati alipotembelea banda la
Shirika hilo kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es
salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerereili kujionea
shughuli mbalimbali wanazozifanya.
Balozi
wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi
kuhusu mradi wa uzalishaji wa chuma ghafi eneo la Maganga Matiti ,
Ludewa mkoani Njombe jijini Dar es salaam kutoka kwa Meneja wa Mradi
huo Abdallah Mandwanga(kulia) wakati Balozi huyo alipotembelea Banda
la Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwenye maonyesho ya 35 ya
kimataifa ya biashara ya Dar es salaam yanayoendelea katika Viwanja vya
Mwalimu Nyerere. Kushoto ni Meneja Mawasiliano Neema Mbuja. Mradi huo
unasimamiwa na Maganga Matitu Resources Development Limited.
Balozi
wa Ireland nchini Loccam Fullam(katikati) akipata maelezo mafupi
kutoka kwa Mtaalamu wa Miamba(Geologist) wa Kampuni ya TANCOAL Alex
Sosteness(kulia) kuhusu mradi wa machimbo ya makaa ya mawe wa Mbalawala
wilayani Mbinga unaotarajiwa kuanza uchimbaji hivi karibuni.Mtaalamu
huyo alitoa maelezo hayo wakati Balozi huyo alipotembelea NDC kwenye
maonyesho ya 35 ya kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu
Nyerere jijini Dar es salaam. Kushoto ni Meneja Mawasiliano wa Shirika
la Maendeleo la Taifa Neema Mbuja.
Picha na Tiganya Vincent-MAELEZO
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)