Sio siri kwamba upole wa Watanzania
ni miongoni mwa sababu kuu za mabaya mengi yanayotokea huko nyumbani.Na
kama kuna suala linalosikitisha kuhusu mwamko wa Watanzania kudai haki
zao ni tatizo la mgao wa umeme sambamba na ubabaishaji wa hali ya juu
wa serikali na Tanesco katika kushughulikia tatizo hilo.
Sasa hivi,mitandao ya jamii ya
Twitter na Facebook imetawaliwa na malalamiko ya Watanzania wengi
kuhusu mgao.Wengine wanaishiwa na uvumilivu na kuishia kuitukana
Tanesco,kana kwamba matusi hayo yatarejesha umeme.Wengine wamekuwa
wakipeana taarifa kuhusu maeneo ambayo "Tanesco wameshachukua umeme
wao".Kwa kifupi,kinachosikika zaidi ni manung'uniko,lawama,vilio na
hata matusi.Cha kusikitisha ni kwamba hakuna dalili yoyote kutafsiri
malalamiko hayo into vitendo.
Kwa Habari Zaidi Na Chanzo <<<< BOFYA HAPA >>>
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)