Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini David Jairo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
---
NA.MAGRETH KINABO –MAELEZO
Serikali
imesema iko katika mchakato wa kufanya mazungumzo na kampuni ya
Kiserikali ya China Petroleum Oil kutoka China kwa ajili ya kujenga
bomba la kuongeza uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi asilia.
Hayo yalisemwa na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye viwanja vya Mnazimmoja
baada ya kutembelea shughuli za maonyesho za wizara yake katika
maadhimisho ya wiki ya utumishi wa Umma.
Aliongeza
kuwa ili kuharakisha mchakato huo, mazungumzo hayo yanatarajia
kutafanyika wiki ijayo na kampuni hiyo inatarajia kusaidiana na Shirika
la Maendeleo ya Mafuta Nchini (TPDC) ili kuzalisha umeme kwa wingi.
Katibu Mkuu huyo
alisema juhudi zinafanyika ili kuwezesha upatikanaji wa umeme wa gesi
kupitia nishati hiyo kwa wingi, ambapo ili kutekeleza mpango huo,
itakopa kiasi fedha dola za Marekani milioni 778 kutoka serikali ya
China.
Aliongeza kuwa
gesi asilia inayozalishwa na mitambo ya Songosongo hailitoshelezi
mahitaji ya kuzalisha umeme kwa wingi na matumizi mengine.
‘Tunataka kujenga
bomba la inchi 30 kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ili kuweza
kupata gesi ya kuzalisha umeme mwingi ikiwezekana na matumizi ya
majumbani,” alisema Jairo.
Akizungumzia
kuhusu suala la upatikanaji wa umeme wa uhakika alisema serikali
imeweka utaratibu hivyo imejiandaa kuondokana na tatizo ndani ya
kipindi cha miaka miwili au mitatu ijayo.
Aidha Katibu Mkuu huyo aliongeza tayari kampuni ya Symbion Power inazalisha umeme wa MW 75.
Ufafanuzi huo
ulitolewa na Jairo kufuatia malalamiko kutoka kwa wananchi waliokuwa
wanatembelea wizara hiyo, ambapo pia walilalamikia tatizo la kutozwa
ushuru wa REA na EWURA kama alivyoelezwa na Mjiolojia Mkuu kutoka
wizara hiyo, Habbas Ngulilapi .
Jairo alisema ushuru huo unatozwa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini.
Kwa upande wa
madini alisema tatizo la mgogoro wa mgodi wa Nyamongo uliopo Tarime,
serikali inalitafutia ufumbuzi tatizo hilo kwa kushirikisha wadau
mbali mbali.
Hata hivyo aliwataka wananachi kuelwa suala la uwekezaji kwa kuwa ni muhimu kwa taifa .
Alisema
uwekezaji unaogeza mapato kwa nchi ikiwemo maendeleo, hivyo wawatumie
Wabunge, Wakuu wa Wilaya , Madiwani , Viongozi wa Serikali za Mitaa ili
kuweza kupata elimu juu ya umuhimu wa wawekezaji.
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)