Nchimbi, alimhoji waziri mwenzake nje ya ukumbi wa bunge, Dodoma leo saa 5:06 asubuhi lakini Ngeleja hakutoa jibu lolote, zaidi alihamisha somo na kuanza kuzungumzia habari nyingine.
Hata hivyo, mpiga picha wetu ‘alipowafotoa’ wakiwa katika hali hiyo, Nchimbi alisisitiza: “Vizuri kabisa, jana Songea nzima haikuwa na umeme, inabidi Ngeleja atoe majibu ya kueleweka.”
Nchimbi alisema, pamoja na ukweli kuwa Ngeleja ni memba mwenzake katika Baraza la Mawaziri, bado ana kila sababu za kuhoji kitendo cha kukatika umeme jimboni kwake.
Waziri Nchimbi ni Mbunge wa Songea Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.
Picha/Habari Luqman Maloto, Dodoma





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)