Meneja
wa Standard Printers, John Mcharo, (wa pili kulia) akimuonesha mabati
maalumu ya kuchapishia magazeti Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa Chama
Cha Mapinduzi (MNEC), Nape Nnauye, (wa pili kushoto) alipotembelea
kiwandani kuona shughuli za uchapishaji wa magazeti ya Serikali ya
Daily News, Sunday News, HABARILEO na HABARILEO Jumapili. Kushoto ni
Kaimu Mhariri Mtendaji, Mkumbwa Ally na Msanifu Kurasa, Geoffrey
Ng'humba.Picha na Yusuf Badi
--
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Nape Nnauye, amempongeza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, Freeman Mbowe, kwa kusikia mwito wa chama hicho na kuamua kurudisha gari la Serikali alilokuwa akilitumia.
Nape ambaye yupo katika ziara ya kutembelea vyombo vya habari nchini, amemtaka Mbowe kuendelea kutekeleza mwito wa CCM wa kuhakikisha wafanyakazi wa Chadema, akiwamo Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, wanalipa kodi inayotokana na kipato chao (PAYE).
Nape alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akijibu swali baada ya kuzungumza na uongozi wa Kampuni ya Tanzania Standard Newspapers Ltd (TSN), inayochapisha magazeti ya Daily News, Sunday News, HABARI LEO na HABARILEO Jumapili.
“Anaona aibu kutembelea gari lililonunuliwa na walipa kodi wakati Chadema hailipi kodi, ndiyo maana karudisha kwa kukosa uhalali wa kulitumia, ni vema atekeleze mwito wa kulipa kodi na akimaliza, tutamwambia mengine ili wajisafishe,” alisema Nape
kwa Habari zaidi <<<< BOFYA HAPA KWA UTAMU ZAIDI >>>>

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)