Mkurugenzi
wa Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) Dr Raynold Mfungahema akitoa mada kwa wadau wa Teknohama katika
mkutano ulioanyika leo jijini Dar es Salaam
Katibu
mkuu Wizara ya Sayansi na Teknolojia, Dr Florans Turuka akizungumza
leo mchana katika mkutano wa Wadau wa Teknohama uliofanyika makao makuu
ya mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) jijini Dar es Salaam.Turuka
alisema kuwa Wizara ya Mawasilian kwa kushirikiana na wadau ipo katika
mpango mkubwa wa kupeleka Teknolojia ya mawasiliano vijijini kwa lengo
la kuharakisha maendeleo kwa jamii ya Kitanzania inayoishi vijijini.
Kushoto ni Dr Raynold Mfungahema, Mkurugenzi wa watumiaji wa mawasiliano
TCRA. Mwingine ni Injinia Denis Libena kutoka ICT.
Wadau wa Teknohama wakiwa katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.Picha na Mdau Victor Makinda
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)