Pages

MAKAMU WA RAISI DKT BILAL AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI SONGEA JANA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akibonyeza kitufe kuashiria kuzindua rasmi maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanayofanyika kitaifa mjini Songea mkoani Ruvuma. Sherehe hizo zimeanza jana Juni 01, katika Uwanja wa Majimaji. Kulia ni Mke wa Makamu wa Rais Mama Zakia Bilal na (katikati) ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dkt. Christine Ishengoma. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Asasi isiyo ya Kiserikali ya Mkoa wa Ruvuma, Methord John, kuhusu uzalishaji wa matofali yanayochomwa kwa kutumia Makaa yam awe, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika sherehe za uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani zilizoanza mjini Songea mkoa wa Ruvuma, kwenye Uwanja wa Majimaji.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Songea (Songea Girls) wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo. Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Songea (Songea Girls) wakiwa ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hizo.


Picha Na Muhidin Sufiani - VPO

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)