DIAMOND KUPOROMOSHA SHOW LA NGUVU NDANI YA USIKU WA KOPO MJINI DODOMA TAREHE 4 JUNE - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

DIAMOND KUPOROMOSHA SHOW LA NGUVU NDANI YA USIKU WA KOPO MJINI DODOMA TAREHE 4 JUNE

Baada ya kuitambulisha vyema Usiku wa Kopo kwa wakazi wa Dodoma na viunga vyake, Kampuni ya Entertainment Masters Limited magwiji wa burudani nchini, wameamua kuongeza burudani kwa kumshusha rais wa wasafi Diamond Platinum kwenye shoo maalum kwa ajili ya wakaazi wa Dodoma.
 
Usiku huu maalum ujulikanao kama usiku wa Kopo itatawaliwa na nderemo, muziki na vinywaji mbali mbali vya kopo. Lengo haswa ni kuwapa wakaazi wa Dodoma burudani. Usiku wa Kopo na Diamond itafanyika tarehe 4 Juni 2011 katika Ukumbi wa Royal Village.
 
Mbali na burudani toka kwa Diamond Platinum, pia kutakuwepo na burudani mbalimbali ili kukidhi kiu ya burudani ya wakaazi wa Dodoma.
Pia kwa kutambua ya kwamba wanafunzi wa vyuo mbali mbali wanahitaji burudani, EML itatoa usafiri wa kwenda na kurudi kwenye kila chuo.
Usiku wa Kopo itawakutanisha wanafunzi wa vyuo na kuwapa fursa ya kubadilishana mawazo.
 
Muziki katika Usiku wa Kopo itaporomoshwa na MaDJ toka Club Maisha ya jijini Dar es Salaam. Madj hao mahiri ni DJ Zero, DJ S-Dizo na Hyperman HK. Mbali na burudani mbalimbali pia kutakuwepo na zawadi kutoka kwa 

Wadhamini.
 
Penniel Mungilwa
 
Meneja Uhusiano

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages