Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda
akiwaonyesha waheshimiwa wabunge Kombe ambalo Ofisi ya Bunge imeshinda
katika Maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma yaliyofanyika jijini Dar es
Salaam kwa kushirikisha taasisi mbalimbali za Umma kutoka barani
Africa na kufikia kilele wiki iliyopita. Katika Maonyesho hayo Ofisi ya
Bunge imekuwa mshindi wa Pili katika nafasi ya banda bora kwa utoaji
bora wa huduma hususani katika kuelezea Kazi za Bunge, Muundo wake,
Mamlaka ya Bunge nk. Kushoto ni Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel.
Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)