Shoto
Shaban akisindikizwa rokapu ya Mahakama ya Njombe baada ya kuhukumiwa
Jana Mahakama ya wilaya ya Njombe imemfunga jela mwaka mmoja mtuhumiwa
wa kesi namba 223 ya mwaka 2009 Bw. Shoto Shaban ambaye alikuwa
akikabiliwa na kesi ya kuwapiga wanahabari watano kwa mapanga juni 16
mwaka 2009 walipokwenda kufuatilia sakata la kufungwa kwa kiwanda cha
Chai Lupembe Hukumu hiyo imetolewa leo baada ya kesi hiyo kukaa
mahakamani kwa takribani miezi 23 toka ilipoanza kusikilizwa mbele ya
hakimu Abeididom Chanjarika wa mahakama ya wilaya ya Njombe na Mei 30
mwaka huu ndio ilikuwa ni siku ya mwisho kwa mashahidi kutoa ushahidi
wao .Wahabari waliotendwa unyama huo wa kukatwa mapanga ni pamoja na
Dotto Mwaibale (Jambo leo), Betty Kagonga (Tanzania Daima) Mussa Mkama
(mwananchi) Calros Mtoya (majira) na mpiga picha wa kujitegemea Peter
Mtitu.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)