Wazee wa iliyokua Jumuhia ya Africa Mashariki, wakimpepea mwazao mzee Magenge Alver (90) baada ya kuzimia nje ya Mahakama Kuu Jijini Dar es Salaam leo mchana baada ya kuambiwa kuwa rufaa ya madai yao imetupiliwa mbali. Wazee hao hadi hivi sasa bado wamefunga njia hiyo jambo ambalo limesababisha msongamano mkubwa wa magari na kufanya magari yote kushindwa kupita njia hiyo, ambapo askari wa kutuliza ghasia FFU, wamefika eneo hilo muda mchache uliopita na kuanza kuwatawanya kwa maji ya kuwasha. Mzee Rashidi Matema akionyesha msisitizo mbele ya polisi kwa kugagaa chini.
-
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)