TUMBAKU YA TANZANIA YAPATA SOKO NCHINI CHINA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

TUMBAKU YA TANZANIA YAPATA SOKO NCHINI CHINA

  Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akifafanua jambo katika Mkutano huo.
 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami ( Kulia) akiagana na kiongozi wa Ujumbe wa wafanyabiashara kutoka China Bw Zhu Jineng,mara baada ya mazungumzo yao ofisi kwake.

 Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami akiwasikiliza wageni wake (Kushoto)  wakieleza mikakati yao katika biashara ya kununua Tumbaku nchini. Kulia ni baadhi ya maofisa wa Wizara ya Viwanda na Biashara.
---
Tumbaku inayozalishwa nchini Tanzania imepata soko nchini China na kuondoa wasiwasi wa kukosa soko uliotanda miongoni mwa wakulima wa zao hilo katika mikoa mbali mbali.


Habari hiyo njema kwa wakulima wa Tumbaku imebainishwa Jijijini Dar es salaam leo na ujumbe wa Wafanyabiashara kutoka nchini China wenye nia ya kununua Tumbaku hiyo, walipomtembelea Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyrill Chami ofisini kwake.


“Sisi ni wafanyabiashara, tumepokea ombi la serikali ya Tanzania kupitia kwako Mh Waziri wa Viwanda na Biashara ulipowasiliana na Ubalozi wetu kuhusu kutafuta soko la Tumbaku kutokana na mavuno mazuri waliyopata wakulima wenu. Kwa kuanzia, tunao uwezo wa kununua tani elfu 60 za tumbaku ya Tanzania, tunaomba serikali zetu ziwasiliane na kutuwezesha kufanikisha mpango huu” amesema Bw Zhu Jineng, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara hao kutoka China.


Akijibu maombi hayo, Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Cyril Chami amesema, serikali ya Tanzania itaunga mkono mpango huo ili kuinua hali za wakulima wa zao la tumbaku nchini. Ameongeza kuwa, pamoja na kupata soko la nje, serikali pia itaendelea kuvilinda Viwanda vya ndani ili vipate malighafi ya kutosha kuviwezesha kuendelea na uzalishaji na kuchangia pato la Taifa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages