“Rekodi” ya shuffle yang’arisha
tangazo la
Vodacom
Dar es Salaam.Mei.30. 2011. Kampuni
ya Vodacom Tanzania
imeanza
kutoa matangazo mapya ya televisheni yanayoendana na azma yake ya kuleta
mapinduzi katika sekta ya mawasiliano ya simu nchini baada ya kufanya
mabadiliko ya rangi kutoka buluu kuwa nyekundu pamoja na nembo ya
biashara.
Katika tangazo jipya la kampuni hiyo
lililonza kurushwa
hewani hivi karibuni na vituo mbalimbali vya televisheni nchini na
kupatikana
pia katika mitandao ya kijamii ya intaneti – blogs mapinduzi ya
utayaraishaji
na ubunifu katika matangazo ya biashara vinaonakana.
Aidha kivutio kikubwa katika tangazo
hilo ni picha za
tamasha la kipekee la uchezaji wa muziki maarufu wa kisauzi - Koito
ambapo lililenga kuvunja rekodi ya dunia ya idadi ya watu waliojikusanya
na
kucheza muziki kwa pamoja kwa wakati mmoja.
Tamasha hilo la wazi la aina yake
lililohudhuriwa na maelfu
ya wananchi wa kada mbalimbali lilifanyika Februari mwaka huu katika
fukwe ya
bahari ya Hindi eneo la Kigamboni jijinjni Dar es salaam ambapo bila kujali
wingi huo wote walijipanga katika mistari iliyounda msitari mirefu
isiyonakifani
na kucheza muziki wa Koito kwa pamoja.
Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa
Vodacom Tanzania,
Mwamvita Makamba, amesema kuanza kurushwa kwa tangazo hilo ni mwanzo wa
utekelezaji wa azma ya Vodacom Tanzania kuleta mapinduzi ya jumla katika
sekta
ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini yanayokidhi kubadilika kwa sura
nzima
ya Vodacom Tanzania.
Mwamvita amesema Vodacom Tanzania baada
ya kufanya
mabadiliko katika rangi na nembo yake ya biashara kinachofuata sasa ni
kwa
watumiaji wa huduma hizo kunufaika na mabadiliko hayo kuanzia ubora wa
huduma
na namna ya kufikishiwa ujumbe wa upatikanaji wa huduma hizo na njia
mpjawapo
ni matangazo ya biashara
“Ukiangalia tangazo letu jipya utaona
ni jinsi
gani mapinduzi makubwa ya ufikishaji ujumbe kwa wananchi yanavyoanza na
hiyo
ndio azma yetu kwa sasa wengi walikuwa wanajiuliza ni kwa vipi tumeamua
kuwa na
vibonzo katika matangazo yetu ile ni njia mojawapo lakini njia nyingi
zaidi
zeney ubunifu, uhalisia na ubora wa hali ya juu zinafuata na wadau wetu
watazifurahia”alisema
Mwamvita.
Alisema Vodacom Tanzania imejipanga
kuhakikisha kila hatua
inayoipiga kwa sasa inaendana na ujumbe wa mabadiliko yaliyofanyika hivi
karibuni ndani ya kampuni hususan mabadiliko ya rangi.
Katika tangazo hilo jipya Vodacom
Tanzania inawakumbusha
wadau huduma mbalimbali inazozitoa kwa ubora wa hali ya juu ikiwemo
sauti na data
na jinsi huduma hizo zinavyounganisha jamii mbalimbali kwa
wepesi,urahisi
na uharaka zaidi ya mitandao minginenchini.
“Tumefurahi kwamba wadau wetu na
wananchi kwa ujumla
wamepokea mabadiliko yetu katika mtazamo mzuri na kwa furaha na Vodacom
Tanzania kubakia kuwa mtandao chagua bora zaidi kwa kada zote nchini
lakini
kwetu tunatambua nini zaidi tunawaandalia kukidhi mahitaji yao katika
ubowa wa
hali ya juu na kadri ziku zinavyosonga mbele wataendelea kuwa watu wa
kujivunia katika soko la huduma za simu za mkononi nchini”alisisitiza
Mwamvita.
Mabadiliko ya rangi katika Vodacom
Tanzania yana maana kubwa
katika utoaji huduma za kampuni hiyo sokoni lengo kuu ni kuwafanya
wateja wa
kampuni hiyo kuwa katikati ya mipango yote ya kampuni pamoja na
utekelezaji
wake chini ya kauli mbiu ya Kazi ni kwako ikilenga kuwapa
nguvu
na mamlaka zaidi wateja katika kuchagua na kurahisisha maisha kupitia
huduma za
Vodacom.
mwisho
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)