Washitakiwa wa wizi wa fedha za EPA, Rajabu Maranda (kulia) na binamu yake Farijala Hussein, wamekuwa washitakiwa wa kwanza kubebeshwa msalaba wa hukumu ya kesi iliyokuwa ikiwakabili baada ya kutiwa hatiani na kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka mitano. Washitakiwa walikuwa wakishitakiwa kwa makosa zaidi ya manne tofauti ambayo yote walitiwa hatiani kwa kuhukumiwa miaka kati ya miwili na mitano, kwa kuwa adhabu zote zinakwenda pamoja watatumikia adhabu ya juu ambayo ni miaka mitano. Aidha, wametakiwa kuzirejesha fedha zote walizojipatia isivyohalali na wakishindwa watafilisiwa mali zao zote. Hali mahakamani hapo Kisutu, ilikuwa ni ya majonzi na vilio kwa ndugu na jamaa wa washitakiwa mara baada ya hukumu hiyo kutolewa.......NEXT!!
..wakiangalia raia waliofurika mahakamani kwa jicho la mwisho!
...wasikilizaji wa hukumu
washitakiwa mbele ya wanahabari mara baada ya hukumu kutolewa
....ni kilio kwa familia ya akina Maranda (pichani juu na chini)
mmoja wa wanafamilia ya akina Maranda katika lindi la mawazo nje ya mahakama
wakili wa utetezi, Majura Magafu....ameshindwa na jamhuri.
wakili Magafu ameahidi mbele ya wanahabari kukata rufaa
kazi mliyotutuma tumeimaliza wananchi...baadhi ya jopo la mahakimu wakitoka nje ya eneo la kisutu.
PICHA: Dastan Shekidele na Richard Bukos/GPL
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)