MAPACHA WALIOUNGANA WAGOMA KUTENGANISHWA - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

MAPACHA WALIOUNGANA WAGOMA KUTENGANISHWA



Ganga na na Jamina (39) 
Nchini India kuna mapacha wa ajabu ambao umaarufu wao unaendelea kukua taratibu, labda baada ya kuja kugundua kuwa jinsi walivyo inaweza kuwa dili kwao.
Mapacha hao Ganga na na Jamina ambao wana umri wa miaka 39 sasa, wameungana kuanzia sehemu ya kiuno huku kila mmoja akiwa na mguu mmoja na miguu yao ya pili imeungana na kuform mguu wa tatu ambao wanautumia wote wawili, hii ikiwa na maana wana miguu mitatu kwa ujumla wao.
Daktari mmoja nchini marekani, Dr James Stein, ambaye amespesholaizi katika kufanya operesheni za kutenganisha mapacha walioungana, anadai kuwa anaweza kuwatenganisha ili kila mmoja ajitegemee bila madhara yoyote kutokea,lakini cha ajabu wenyewe wanasema hawataki,kwani hawaoni tatizo lolote la wao kuwa katika hali hiyo.
Wanashangaa watu wanaowashangaa kuwa wao ni viumbe wa ajabu. Wao wanasema wao ni binadamu wa kawaida tu kama wengine na wana hisia kama watu wengine.
Ganga na Jamina, hujiingizia pesa nyingi kutoka kwa watu wanaowalipa ili tu kuwashangaa, pesa wanayoitumia kulisha familia yao ya kimaskini inayofikia watu 22.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages