Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akitembelea mahema ya wahanga 80, waliopatwa na janga la kuchomewa nyumba zao na watu wasiojulikana eneo la Pwani Mchangani, ambapo hadi sasa idadi kubwa ya watu hao wanaishi katika mahema mawili yaliyojengwa eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akipanda mti ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja eneo la Mtowapwani, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali katika mkoa huo jana Mei 22.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akiweka udongo baada ya kupanda mti ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti katika Mkoa wa Kaskazini Unguja eneo la Mtowapwani, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali katika mkoa huo jana Mei 22.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akitembelea mahema ya wahanga 80, waliopatwa na janga la kuchomewa nyumba zao na watu wasiojulikana eneo la Pwani Mchangani, ambapo hadi sasa idadi kubwa ya watu hao wanaishi katika mahema mawili yaliyojengwa eneo hilo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akishiriki katika dua maalumu ya kumuombea marehemu , Mole Juma Shamte, aliyekuwa Diwani mstaafu wa CCM Kata ya Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, aliyefariki dunia jana Mei 22 katika Kijiji cha Shingwi, wakati Makamu alipofika kutoka mkono wa pole kwa familia ya marehemu. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Pembe Juma Hamis (kushoto) ni Baba wa marehemu, Juma Shamte Nyange.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akitoa mkono wa pole kwa Juma Shamte Nyange, ambaye ni baba mzazi wa marehemu, Mole Juma Shamte, aliyekuwa Diwani mstaafu wa Kata ya Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, aliyefariki dunia jana Mei 22 katika Kijiji cha Shingwi, wakati Makamu akiwa njiani kuelekea katika shughuli za ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya serikani Mkoani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Juma Shamte Nyange, (wapili kushoto) ambaye ni baba mzazi wa marehemu, Mole Juma Shamte, aliyekuwa Diwani mstaafu wa Kata ya Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, aliyefariki dunia jana Mei 22 katika Kijiji cha Shingwi, wakati Makamu alipofika kutoka mkono wa pole kwa familia ya marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Vyumba saba vya Madarasa ya Shule ya Sekondari Nungwi, kakati akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali mkoa wa Kaskazini Unguja jana Mei 22.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akionyeshwa sehemu ya madawati yaliyotolewa msaada na wafadhili wa ujenzi wa vymba vya madarasa, wakati alipofika katika shule ya Sekondari Nungwi kuzindua Vyumba saba vya madarasa, akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali mkoa wa Kaskazini Unguja, jana Mei 22.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Nungwi, wakati alipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuzindua vymba saba vya madarasa, wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya Serikali katika mkoa wa Kaskazini Unguja jana Mei 22.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mzee wa kijiji cha Kipange, baada ya kuweka jiwe la msingi katika jingo la Ofisi ya CCM Tawi la Kipange Mkoa wa Kaskazini Unguja jana Mei 22
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohamed Gharib Bilal, akitoa mkono wa pole kwa Juma Shamte Nyange, ambaye ni baba mzazi wa marehemu, Mole Juma Shamte, aliyekuwa Diwani mstaafu wa Kata ya Mkwajuni Mkoa wa Kaskazini Unguja, aliyefariki dunia jana Mei 22 katika Kijiji cha Shingwi, wakati Makamu akiwa njiani kuelekea katika shughuli za ziara yake ya kukagua maendeleo ya miradi ya serikani Mkoani humo. Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)