Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TanzaniaDkt.Mohamed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti,inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi.Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25.
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, alipokuwa akifungua warsha hiyo leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Profesa Amandina Lihamba,wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,mara baada ya kufungua Warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti,inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam,Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohamed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na washiriki baada ya kufungua rasmi warsha ya siku mbili kuhusu Utafiti, inayovishirikisha vyuo vikuu vya Dar es Salaam, Chuo cha Afya na Tiba Muhimbili na Chuo cha Ardhi. Warsha hiyo imeanza leo Mei 24 katika Hoteli ya White Sands na itamalizika kesho Mei 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya kifo cha mke wa kwanza wa Balozi George Kahama, Mama Maria Kahama, aliyefariki dunia Mei 19, 2011 na kuzikwa juzi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisalimiana na watoto wa Marehemu Mama Maria Kahama,aliyekuwa mke wa kwanza wa Balozi George Kahama,wakati alipofika kutia saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu ADA Estate Kinondoni Dar es Salaam leo Mei 24.Picha na Muhidin Sufiani-Ofisi Ya Makamu Wa Rais
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)