Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihojiwa na waandishi wa habari baada ya kufungua mkutano huo wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Samwel Muro, wakati alipotembelea banda lao la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kuvaa miwani ili kuweza kuona picha iliyokuwa ikionyeshwa ukutani kupitia Screen na Projector (Animation Fils) , wakati alipotembelea Banda la maonyesho baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam jana Mei 25. Kushoto ni Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka na Waziri wa Elimu na Mafunzo, Shukuru Kawambwa (kulia) ni Mkurugenzi wa Designmate Animation Films, Colonel Basavaraj
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Imelda Lutebinga na Langton Chibura wakati alipotembelea Banda lao la maonyesho la SEACOM Tanzania Ltd, baada ya kufungua mkutano wa sita wa Kimataifa wa Afrika kuhusu Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ya Ustawi, Elimu na Mafunzo (ICT), uliofunguliwa jijini Dar es Salaam jana Mei 25
Picha/Habari VPO-Photographer.





No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)