Habari zilizopatikana jana usiku zinadai kuwa watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha za moto, walifunga barabara eneo la mlima wa Kitonga na kuteka magari zaidi ya 20.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 8 usiku na kudumu kwa zaidi ya saa 1 baada ya baadhi ya madereva waliweza kupiga simu kituo cha polisi mjini Iringa na hatimaye askari kufanikiwa kufika eneo hilo la tukio kutoka kituo cha Ilula ambao walifika kwa wakati na kufanikiwa kunusuru usalama wa madereva ambao walikuwa wametekwa.
Mmoja kati ya madereva aliyenusurika kutekwa katika tukio hilo aliueleza mtandao wetu kuwa yeye alikuwa na gari jipya lenye namba za IT akitokea Dar es Salaam kwenda Tunduma akiwa na wenzake ambao walitangulia na kukumbwa na mkasa huo.
Dereva huyo alisema yeye na baadhi ya madereva walipoona hali hiyo walirudi nyuma hadi Hotel ya Kitonga hadi majira ya saa 10 usiku baada ya polisi kufika eneo hilo na kuwatawanya majambazi hayo na kuwahakikishia usalama madereva hao japo alidai kuwa usafiri katika barabara hiyo ulisimama kwa masaa kadhaa kwa kuhofia usalama.
Habari Kwa Hisani Ya Sufiani Mafoto.

No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)