Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwakaribisha viongozi wa Jukwaa la Katiba walipowasili ofisini kwake leo kujadili njia bora zaidi ya kuunda tume ya kukusanya maoni ya wananchi kwa ajili ya Katiba mpya ya Tanzania.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Jinsia nchini Bi.Usu Mallya (kulia) na Mwenyekiti wa TAMWA Bi Annanilea Nkya wakichangia maoni kwenye uundwaji wa Tume hiyo. Kwa pamoja wanaharakati hao wamempongeza Spika kwa hatua aliyochukua ya kukutana na wadau mbalimbali na kuweka mwanzo mzuri wa ukusanywaji wa maoni.
Wajumbe wa Jukwaa la Katiba wakimsikilza Mhe. Spika kwa makini.
Wajumbe wa TAHILISO.
Viongozi wa mtandao wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu (TAHILISO) wakifuatilia mjadala.
Viongozi wa Jukwaa la Katiba wakiongozwa na Mwanaharakati machachari Bw. Deus Kibanga (kulia).Picha na Prosper Minja-BUNGE
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)