Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na kumkaribisha ofisini Mwenyekiti wa TLP Mhe. Auugustine L. Mrema (Mb) alipowasili ofisini hapo kuhudhuria mjadala wa maboresho ya muswada wa Tume ya kuratibu mchakato wa Katiba mpya Jana.
Ujumbe wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ukiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama Tanzania Bara Mhe. Pius Msekwa, (kulia), Naibu Katibu Mkuu Taifa Capt. John Chiligati (katikati) na Katibu Mwenezi wa Chama Bw. Nape Nauye wakiwa katika ofisi ya Spika wa Bunge jana. Huu ni mwendelezo wa mjadala wa kupata tume ya kuratibu mchakato wa katiba mpya.
Mwenyekiti wa DP Mchungaji Christopher Mtikila akitoa msimamo cha chama chake kwenye mchakato wa kuunda tume ya kukusanya maoni. DP inasisitiza kwamba Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania haiwezekani ila ya Tanganyika tu.
Ujumbe uliondamana na Mhe. Mrema ukimsikiliza Mhe. Spika. Kutoka Kulia ni Mwenyekiti wa TLP Mhe Augustine L. Mrema, Katibu wa Chama…., Mkurugenzi wa Utawala…. Na Katibu wa Wanawake TLP Taifa Bi Nancy Mrikaria.
Viongozi wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala wakifuatilia mjadala kwa makini. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Pindi Chana, Makamu Mwenyekiti Mhe. Angela Kairuki na Mjumbe wa Kamati Mhe. Musa Ally Kombo, MB.Picha na Prosper Minja-Bunge
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)