chwaaaaaaaarrrrrrrrr
Waaa!
Halafu bonge la msamba!
Wilson Jumanne ni mtoto mwenye umri wa miaka 12 tu, anayesoma darasa la tatu, katika shule ya msingi Boma, Ilala jijini Dar es Salaam, ambaye Blogu ya Chachandu Daily imekumbana naye, na kuaminia kwamba ni 'mari' wa kutosha katika medani ya uchezaji wa sanaa na mapigano ya Kung Fu.
Kwa mwili ni mtoto anaonekana kuwa mtoto mdogo, lakini ukimuona ni mwenye mwili ulio 'stebo' na makini kiasi cha kuumiliki vema mchezo huo wa Kung Fu, ambao ni maarufu katika nchi za Asia, hususan, China na Japan.
Akizungumza na Chachandu Daily, mtoto huyu alisema, ameanza kufundishwa Kung Fu miaka mitatu iliyopita, akiwa jijini Nairobi Kenya alikokuwa anaishi na Shangazi yake ambaye kutokana na kufariki dunia imebidi mtoto huyo arudi Dar kwa baba yake.
Ni mtoto mwenye nidhamu, msikivu lakini pia anayeshika vema masomo darasani, ambapo kwa mujibu wa baba yake amabaye naye ni mahiri kwa mchezo huo, Master Jumanne, mwaka jana alikuwa mtoto wa nne katika mtihani wa darasa la pili.
Katika picha zifuatazo, mtoto huyo ambaye sasa yupo daraja la mkanda mwekundu 'RED BELT' katika Kungu Fu ya watoto, anaonyesha umahiri wake katika miondoko ya ' Taichi Chwan' yaani 'kilele kirefu', wakati wa sherehe za maadhimisho ya wiki ya Jumuia ya Wazazi yaliyofanyika leo kwenye ukumbi wa CCM, Ilala Kota.
Na Chachandu Daily
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)