VODACOM YAJA NA NEMO NYEKUNDU - LUKAZA BLOG

All You Want is Here | Chochote Unachohitaji Utakipata Hapa

Habari Mpya

VODACOM YAJA NA NEMO NYEKUNDU

 Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom ambayo ni kampuni kubwa ya simu za mkononi nchini  Dietlof Mare  akiongea leo asubuhikwneye uzinduzi wa Nembo mpya ya Vodacom
----
Dar es Salaam, April 3, 2001: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania leo imezindua Nembo yake mpya kuashiria mabadiliko makubwa ndani ya kampuni hiyo na utendaji wa shughuli zake nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom ambayo ni kampuni kubwa ya simu za mkononi nchini  Dietlof Mare alisema kuwa mabadiliko hayo ya kwanza na ya aina yake kufanywa na Vodacom yataibadili nembo yake kutoka rangi ya bluu ya sasa na kuwa na Rangi  Nyekundu na kwamba zoezi hilo linakusudia kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zake.

“Naamini mabadiliko lazima yaanzie kwetu. Tunajipanga upya bila kupoteza thamani bali kuongeza ubora wa bidhaa na huduma zetu," alisema Dietlof Mare.

Mare alifafanua kuwa mabadiliko hayo yanalenga sio tu kuwapa wateja wa Vodacom huduma bora zaidi, lakini pia ya haraka kuweka hai na kutimiza ahadi ya kampuni hiyo kwa wateja wake kutoa huduma kulingana na thamani halisi ya fedha za wateja.

"Haya si mabadiliko ya nembo na rangi zetu pekee, bali kampuni nzima na jinsi inavyofanya biashara na kuhudumia wateja wake. Ni mabadiliko makubwa kuliko ya rangi, ni mabadiliko ya  mtazamo na mwelekeo kwa Vodacom katika zama mpya ambapo mawasiliano si anasa tena bali ni hitaji la msingi,”alisema Mare na kuongeza:
“Tunataka kuunganisha nchi nzima kwa mawasiliano ya Vodacom, si mijini  pekee bali maeneo yote hata vijijini na haya ndiyo mabadiliko tunayolenga na tunayowaletea."

Alisema mtandao wa kampuni yake, huduma na thamani ni maeneo matatu muhimu yanayogusa wateja wa Vodacom ambayo yamekuwa yakiboreshwa kwa nyakati tofauti pia ni sehemu ya hatua hizo za mabadiliko ndani ya Vodacom.   

Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa sasa ndiyo yenye mtandao mpana zaidi nchini ambapo Mare amesema kuwa wanakusudia kuongoza katika teknoloji na kwamba mabadiliko ya teknolojia yataendelea kuwa sehemu muhimu ya Vodacom kuboresha mtandao wake pamoja na kuendelea kuongoza katika utoaji huduma za fedha kwa simu za mkononi nchini.

Alieleza kuwa Vodacom kama kampuni inayoongoza, inategemea kutimiza matarajio ya wateja wake kwa kutimiza ahadi zake akieleza kuwa mabadiliko yanayoshuhudiwa sasa ni mwanzo wa safari ya mabadiliko makubwa akiahidi kwamba Vodacom itafanya kazi zake kwa kuzingatia sheria, taratibu, uaminifu na kasi ya ajabu.

Mabadiliko hayo yamekuja kufuatia kampuni mama ya Vodafone Group (UK) ya Uingereza kununua asilimia 65 ya Hisa za kampuni ya Vodacom Group (SA) ya Afrikakusini na kuamua Vodacom kutumia nembo ya Vodafone na kauli mbiu ya "Nguvu Kwako"

Mabadiriko hayo ya rangi yataiwezesha Vodacom kuonekana uhalisia wake wakuwa kampuni tanzu ya Vodafone ambayo ni miongoni mwa makampuni yanayoongoza katika nyanja za mawasiliano duniani kote.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)


Pages